Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Yanga wiki hii wanatarajia kutangaza tarehe ya uchaguzi wa kujaza nafasi za uongozi katika klabu ya Yanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Malangwe Mchungahela amesema mchakato huo hautaanza upya, utaendelea pale ulipoishia
Wakati mchakato huo ulipositishwa baada ya baadhi ya wanachama kwenda Mahakamani kuupinga, wagombea walikuwa wakiendelea na kampeni
Hivi karibuni Yanga ilitangaza Kamati yake ya uchaguzi ambayo itashirikiana na ile ya TFF kusimamia uchaguzi huo
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Mh Venance Mwamoto (MB) ambaye anasaidiwa na Mh Seif Gulamali (MB)
Yanga ilishindwa kufanya uchaguzi katika tarehe iliyopangwa awali Januari 13 kutokana na kesi zilizofunguliwa Mahakamani
No comments:
Post a Comment