Mwamuzi wa mechi ya Jana dhidi ya Simba amelaumiwa na Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali 'Bilo'.
Kocha huyo alizungumza mara baada ya mchezo amesema kuwa Mwamuzi aliwabeba na kuwasaidia Simba kupata mabao 2 ambayo alidai hayakuwa halali.
Bilo ambaye alitamba kuwamaliza Simba SC kwenye kipute hicho, anaamini Mwamuzi aliwapa msaada Simba na mechi haikuwa na usawa kiuchezeshaji.
"Tumefungwa lakini Mwamuzi amewasaidia Simba, si mabao sahihi kwakuwa kulikuwa na upendeleo kwao", alisema Bilo
Aidha amesema kuwa anaweza kusema msaada wa refa umewasaidia Simba kuchukua alama tatu ambazo si halali kutokana na namna mchezo ulivyochezeshwa.

No comments:
Post a Comment