Msafara wa kikosi cha Simba umeondoka jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Ijumaa, kuelekea Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC ambao utapigwa siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Jamhuri
Leo jioni Simba inatarajiwa kufanya mazoezi yake ya kwanza katika uwanja wa Jamhuri ambao uongozi wa timu hiyo uliufanyia ukarabati wa sehemu ya kuchezea 'pitch'
Baada ya mchezo dhidi ya Mbao Fc, Simba itaendelea kubaki mkoani Morogoro kuendelea na maandalizi ya mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe
No comments:
Post a Comment