Simba itaweka makazi ya muda mkoani Morogoro ikitumia uwanja wa Jamhuri kwa baadhi ya michezo yake ya ligi wakati wote ambao uwanja wa Taifa utakuwa umefungwa
Katika kuhakikisha uwanja huo unakuwa na hali nzuri, wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba mkoani Morogoro walijitolea kuufanyia ukarabati
Ukarabati uliofanywa ni pamoja na kun'goa magugu, kujaza vifusi sehemu zenye mashimo na kuotesha nyasi pamoja na kumwagilia katika kipindi cha wiki tatu zilizopita
Pia ukarabati umefanywa kwenye vyoo na vyumba vya kubadilishia nguo
Meneja wa uwanja huo John Simkoko amewapongeza Wanasimba kwa jitihada zao za kuuboresha uwanja huo
Simba itaanza rasmi kuutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wake wa nyumbani kesho Jumapili itakapochuana na Mbao Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
No comments:
Post a Comment