We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, March 30, 2019

Chanzo ya mlango wa kizazi ni salama - Makamu wa Rais


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaasa wananchi wote hususani Wazazi kuwapeleka mabinti wao kupata chanjo ya mlango wa kizazi (HPV) ili kuwakinga dhidi ya Saratani ya hiyo. 

Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa mashine mpya za tiba ya mionzi (linear accelerators) katika Taasisi ya Saratani Ocean Road Jijini Dar es salaam. 

Samia amesema kuwa Chanjo ya mlango wa kizazi ni salama na inatumika katika nchi mbali mbali Afrika ikiwemo nchi za Uganda, Rwanda,Afrika Kusini, Zambia na Lesotho, hivyo kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka mabinti wao kupata chanjo hiyo inayopatikana bila malipo. "Kwa maelezo ya Wataalamu wametuhakikishia chanjo hii haina madhara, hivyo basi nawasihi Wazazi na Walezi wenye watoto kuhakikisha binti zetu ambao wengi wapo mashuleni, wanapata chanjo hii " alisema Samia. 

Aidha, Samia amesema kuwa takribani wasichana 507,720 hapa nchini, wamepatiwa chanjo hii ya mlango wa kizazi, huku lengo likiwa ni kuwafikia wasichana 616,734 hadi Disemba 2018, 
Mhe. Samia amesema kuwa nchi ya Tanzania inaripotiwa kuwa na Wagonjwa wa Saratani takribani 42,060, huku wagonjwa 28,610 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ugonjwa huo. 

Samia aliendelea kusema kuwa takwimu za 2018 za hospitali zinazotibu ugonjwa wa Saratani hapa nchini zinaonesha kuwa ni wagonjwa 14,000 sawa na 33.4% ndio wanaofika katika Hospitali ya Ocean road kupata huduma, ambao ni takribani wagonjwa 7600 kwa mwaka. "Takwimu za hospitali zinazotibu ugonjwa wa Saratani hapa nchini za 2018, zinaonesha wagonjwa 14,000 sawa na asilimia 33.4 ndio wanaofika katika Hospitali yetu ya Ocean kupata huduma , ambao kwa mwaka ni 7600, Bugando ni wagonjwa 2790, KCMC 1050, Muhimbili 1321 na Mbeya Rufaa ni 218" alisema Mhe Samia Suluhu...

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list