Niyonzima amesema kuwa wachezaji wa Simba wanatambua ugumu wa hatua inayofuata na kila mmoja akili zake ni kuona namna gani atapata matokeo hivyo ni wakati wao sasa kupeperusha bendera ya Simba kuelekea kwenye mafanikio.
"Tumepenya hatua ya robo fainali kutokana na morali ambayo tulikuwa nayo wachezaji, kushirikiana na kukubali kwamba tunaweza kufanya kitu kikubwa kwa ajili ya Simba na hatimaye tumepata matokeo.
"Kwa sasa hakuna kingine tunachokifikiria zaidi ya kuona timu inapata matokeo kwenye hatua ya robo fainali ambayo tumepambana kuifikia na tumefanikiwa, mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani uwepo wao umetusaidia kwa kiasi kikubwa," amesema Niyonzima.
Simba watamenyana na TP Mazembe kwenye mchezo wao utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Aprili 5 mwaka huu na watarudiana na Mazembe Congo baada ya siku sita.

No comments:
Post a Comment