Serikali ya Rwanda imewasihi Wananchi wake kusitisha ziara zao nchini Uganda baada ya kuishtumu nchi hiyo kuwanyanyasa raia wake wanaoishi ama kutembelea nchini humo.
Uganda imeishutumu Rwanda kufunga mipaka baina ya nchi mbili,lakini Rwanda imekanusha na kusema mipaka iko wazi.
Alhamisi iliyopita mamlaka ya mapato ya Rwanda iliamrisha maroli ya mizigo kutotumia tena mpaka wa Gatuna kwa madai ya shughuli za Ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani 'one stop border' baina yake na Uganda.
Kwa mujibu wa mamlaka ya mapato ya Rwanda Malori yaliombwa kutumia mpaka wa pili wa Kagitumba Kaskazini mwa Rwanda.
Hata hivyo watumiaji wa mipaka hiyo miwili hupendelea njia ya mpaka wa Gatuna kuwa rahisi na fupi kuliko ya mpaka wa Kagitumba.

No comments:
Post a Comment