Katika kampeni ya Tokomeza Zero iliyoandaliwa na DC wa Kisarawe Mh. Joketi Mwegelo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City walihudhuria viongozi mbalimbali wa Serikali lakini pia pamoja na wadau mbalimbali wa Sanaa ikiwemo wasanii na hata watu ambao sio wasanii ila wana umaarufu.
Katika hafla hiyo walifanikiwa kuongea viongozi mbalimbali na wadau mbalimbali katika kutoa ahadi ya kuchangia angalau chochote walichojaliwa nacho kwa ajili ya kupata pesa zitakazo saidia kujenga shule ya kwanza ya bweni ya wasichana katika wilaya hiyo ya kisarawe na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh. Paul Makonda alipata wasaa wa kutoa neno na kuanza kwa kumpongeza sana mama mmoja ambaye alifanikiwa kumsomesha mtoto wake mpaka chuo kikuu hali ya kuwa ni masikini na mama ntilie na hapo ndipo aliposema” Kwa waandishi wa habari watu kama hawa ndio wakupewa vipaumbele sio hao watu wenu kama akina Pierre ambao ni walevi, hatuwezi kuwa na taifa la wajinga, walevi ndio wanakuwa maarufu”
No comments:
Post a Comment