Kikosi cha klabu ya Tottenham kwa mara ya kwanza hii leo kimefanya mazoezi kwenye uwanja wao mpya uliyotengenezwa kwa gharama ya pauni bilioni moja.

Wachezaji wa Spurs wamefanikiwa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, na sehemu nyingine ya uwanja huo kabla ya kuanza kufanya mazoezi kwenye dimba hilo.


Wachezaji wa Tottenham wakifanya ‘warmed’ kwenye uwanja wao mpya

Wachezaji kama Christian Eriksen, Erik Lamela na wengine wakionekana wakifanya mazoezi mepesi mepesi katika dimba hilo

Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza jumla ya mashabiki 62,000 watushuhudiwa ukianza kuchezewa katika mechi ya kwanza dhidi ya Crystal Palace tarehe 3 ya mwezi Aprili.
Siku ya Jumamosi kikosi cha wakongwe wa Tottenham wataanza kuutimia uwanja huo kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Inter Milan.
Tottenham imekuwa ikitumia uwanja wa Wembley katika mechi zake tangu mwezi Agosti mwaka 2017 .

No comments:
Post a Comment