We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, March 26, 2019

PICHA 4: Unahitaji Milioni 500 ili kumiliki daftari lenye ngoma za Lil Wayne

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ unaripoti kuwa kwa mtu yeyote mwenye uhitaji wa kumiliki daftari lililojaa ngoma za Rapper Lil Wayne basi anahitaji kuwa na shilingi milioni 500 za Kitanzania ili kulipata daftari hilo lenye mistari kadhaa. 
Inaelezwa kuwa daftari hilo lenye mistari ya Lil Wayne ambalo aliandika kuanzia mwaka 1999kwa sasa lipo sokoni na linapigwa bei na kampuni ya Moments In Time na kutajwa kufikia dola za Kimarekani 250,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 586 za Kitanzania.
Inaripotiwa kuwa ndani ya daftari hilo kuna mistari ya ngoma kama “We On Fire” na “I Feel” kipindi hicho akiwa na kundi la Hot Boysakiwa na umri wa miaka 17.
Inaelezwa kuwa mmiliki wa daftari hilo kwa sasa ni kijana mmoja ambaye anadai kuwa alilikuta kwenye gari lililokuwa gereji wakati likimilikiwa na Cash Money Records, daftari hilo lilikuwa limelowa maji kutokana na mafuriko yaliyotokana na kimbunga Katrina ambapo vitu vyake vingi vilipata maafa kasoro boksi ambalo lilikuwa na daftari hilo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list