Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa nchi hii ni ya hatari sana na ina wajuaji wengi.
Rais Magufuli amesema kuwa Mkurugenzi amezungumzia suala la kulipa kodi hili ni eneo moja wapo ambalo nchi hii inaibiwa sana.
"Nchii hii ni ya hatari kuna wajuaji wengi katika nchi hii, maajabu mengi yanafanyika mengi Mkurugenzi hapa amezungumzia suala la kulipa kodi hili ni eneo moja wapo ambalo nchi hii inaibiwa sana hata kwenye Tax refund, tax refund nyingi zinazodaiwa ni za foguring," alisema Rais Magufuli wakati akipokea ripoti kutoka TAKUKURU Ikulu jijini Dar Es Salaam.

No comments:
Post a Comment