Mchezaji bora duniani, Lionel Messi amesema kuwa anatamani mpinzani weke mkubwa, Cristiano Ronaldo angelikuwa bado yupo kwenye ligi kuu nchini Hispania, La Liga.
Ronaldo ameondoka Real Madrid na kujiunga na miamba ya soka nchini Italia klabu ya Juventus kwa dau la pauni milioni 100 na kuhitimisha safari yake ya miaka tisa ndani ya La Liga.
Messi na Ronaldo wanaangaliwa kama moja ya wachezaji bora kabisa wa muda wote duniani na kwa sasa Muargentine huyo amesema kuwa anammisi mpinzani wake Ronaldo kwenye ligi ya La Liga.
”Nammisi Cristiano,’, amesema nyota huyo, Messi akikiambia chombo cha habari cha radio FM Club 947 nchini Argentina.
”Juventus amekuwa rahisi kwake kutwaa taji la Champions League tangu kutua kwa Cristiano ndani ya klabu hiyo huku mechi yao dhidi ya Atletico ikiwaongezea kujiamini zaidi.”
Tangu kuondoka kwa Ronaldo klabu ya Real bado haijakuwa kwenye kiwango kizuri, wakati kwenye msimamo ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo kwakuwa na pointi 54 huku wakitolewa kwenye hatua ya 16 ya michuano ya Champions League na kushindwa kabisa kupata mbadala wa nyota huyo raia wa Ureno.
Alipotakiwa ataje mchezaji ambaye anamuona kuwa ni bora aliyewahi kukutana naye kwenye mechi alizopata kucheza nahodha huyo wa Barcelona amesema.
”Si hitaji kumsahau mtu yoyote, lakini nadhani, Neymar, Kylian Mbappe, Eden Hazard, Luis Suarez na Sergio Aguero hawa ni bora sijamtaja Cristiano kwasababu namuweka yeye kwenye nafasi yangu.”
Hata hivyo Messi amesema hayupo fiti kwa asilimia 100, anasema hivi zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kuwavaa Manchester United kwenye robo fainali michuano ya Champions League.
No comments:
Post a Comment