Na Ferdinand Shayo, Arusha
Maelfu ya watu kutoka katika mikoa mitano nchini wamekutana jijini Arusha na kufanya maombi maalumu ya kuomba Mvua zinyeshe kutokana na msimu wa mvua kuchelewa na kuleta hali ya wasi wasi kwa wakulima.
Maombi hayo yamefanyika katika Viwanja vya Magereza Kisongo yakiongozwa na Huduma ya Maombi ya Safina ambapo Wananchi kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na mikoa mingine wamejumuika na kuliombea taifa na taifa jirani la Kenya ambalo baadhi ya maeneo yake yanapitia hali ya ukame.
Mchungaji Jovin Msuya amesema kuwa maombi hayo yanalenga kuombea mvua na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababisha uhaba wa mvua na pia kuwaombea Viongozi wa serikali hususani Raisi John Magufuli ili aweze kuwaongoza vyema Watanzania kuelelekea katika maendeleo hasa ya uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment