We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, March 28, 2019

Kesi ya Bernad Membe dhidi Cyprian Musiba yapigwa kalenda.

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernad Membe, leo ametinga Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kusikiliza kesi yake ya madai ya fidia ya Sh. Bilioni 10 dhidi ya Cyprian Musiba iliyopangwa kusikilizwa mahakamani hapo.
Hata hivyo, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Elinaza Luvanda ilishindwa kuanza kusikiliza madai hayo baada ya mlalanikiwa kuwasilisha maombi ya kuomba kuongezewa muda wa kuwasilisha majibu dhidi ya Membe.

Membe aliyekuwa ametinga shati la rangi nyeupe na suruali nyeusi, alifika mahakamani hapo mapema leo saa 3:00asubuh akiwa na wakili wake Jonathan Mndeme.

Upande wa mlalamikiwa uliwasilisha maombi namba 119/2019  ukiomba kuongezewa muda wa kuwasilisha majibu nje ya muda.

Jaji alisema mlalamikaji atawasilisha majibu ya maombi hayo Aprili 12 na mahakama yake itasikiliza Aprili 17, mwaka huu na kwamba kesi ya msingi itasubiri uamuzi wa maombi hayo utakapotolewa.

Musiba anadaiwa kumtuhumu  Membe  kuwa anamhujumu Rais Magufuli, na kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi ya  kampeni za kugombea urais 2020.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list