We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, March 29, 2019

CUF yazugumzia kuanza kufukuza wabunge wake

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Khalifa Suleiman amesema kuwa msimamo wao ni kutomfukuza Mbunge yeyote ambaye alikuwa upande wa Maalim Seif Hamad na kuongeza kuwa kwa Mbunge atakayeona yuko tayari kuacha ubunge aandike barua ya kujiuzulu.
Khalifa ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na www.eatv.tv juu hatma ya Wabunge ambao walionekana kutounga mkono upande wa Prof Lipumba, wakati mgogoro wa chama hicho ukiendelea.
"Katika mahojiano yangu yote yale, tumesema Wabunge hatuna shida nao yoyote ile, ila tumesema tutawaita kama Wabunge ili waje kutoa ushirikiano," amesema Khalifa.
"Kuhusu Mbunge Katani ambaye alionekana kuwa sio upande wetu hatumfyeki, nachokiamini Katani atatoa ushirikiano, kama anaamini aliingia katika chama ili asipate uongozi basi tunamruhusu kuandika barua ya kujiuzulu Ubunge." ameongeza Khalifa.
Hivi karibuni Khalifa huyo akizungumza na www.eatv.tv alibainisha kuwa chama hicho kipo tayari kushirikiana na vyama vingine ikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kujenga demokrasia Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list