We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, March 26, 2019

Atupwa miaka 30 jela kwa kumbaka mama yake mzazi


Linaweza kuwa ni tukio la kushangaza, lakini ushahidi uliotolewa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Serengeti umethibitisha pasi na shaka kuwa Chora Samson (27), alimbaka mama yake mzazi. 

Hivyo, haikuwa ajabu kwa kijana huyo wa kijiji cha Burunga, kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa hilo la nadra kutokea nchini kumbaka Rhobi Nyang’ombe, mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 65. 

Kabla ya Hakimu Mkazi Ismael Ngaile kusoma hukumu hiyo, mwendesha mashtaka wa Serikali, Renatus Zakeyo aliikumbusha mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 26, 2017 saa 3:00 usiku. 

Zakeyo alidai katika kesi hiyo ya jinai namba 8/2018 kuwa baada ya Chora kukamatwa alifunguliwa kesi na kufikishwa mahakamani, lakini akakana kosa hilo. 

Mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa kitendo alichofanya hakikubaliki katika jamii. 

Alipopewa nafasi ya kujitetea kabla ya hakimu kusoma hukumu, Chora aliiomba mahakama imuonee huruma kwa kumpunguzia adhabu, akidai kuwa hilo ni kosa lake la kwanza na ana watu wanaomtegemea nyumbani kwake. 

Hata hivyo, Hakimu Ngaile alisema utetezi wake hauna nguvu ya kuishawishi mahakama isitoe adhabu kali, na ndipo akamsomea hukumu hiyo itakayomuweka nyuma ya nondo za gereza kwa miaka 30. 

Hakimu alisema milango ya rufaa iko wazi kwa mshtakiwa kama hakuridhika na adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list