Baada ya Mwanamuziki, Harmonize kugawa vitambulisho kwa wajasiriamali 200 wa Kariakoo Dar es salaam. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amempongeza msanii huyo.
Msigwa amesema kuwa msanii huyo amemuunga mkono Rais Magufuli baada ya kugawa vitambulisho hivyo.
"Mwanamuziki Harmonize amuunga mkono Mhe. Rais Magufuli. Agawa vitambulisho kwa wajasiriamali 200 wa Kariakoo Dar es salaam," aliandika Msigwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
"Haya ndio mambo Konde Boy. Mwenyezi Mungu akubariki na abariki kazi ya mikono yako."

No comments:
Post a Comment