We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, March 29, 2019

ALICHO KISEMA JOSHUA NASSARI BAADA YA MAHAKAMA KUTOA MAAMUZI JUU YA KESI YAKE YA UBUNGE

Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, amesema atakata rufaa baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma, kutupilia mbali maombi yake ya kupinga kuvuliwa Ubunge na Spika Job Ndugai kwa makosa ya utoro bungeni.


Joshua Nassari
Uamuzi wa Nassari umeelezwa na Wakili wake, Fred Kalonga muda mfupi baada ya Mahakama hiyo kufanya maamuzi yake ambapo ameeleza pamoja na kupokea maamuzi ya mahakama wataenda ngazi ya juu ili kupata haki.
Mapema leo, Machi 29, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ilitupilia mbali ombi la mbunge huyo la kufungua kesi ya msingi ya kutengua uamuzi wa spika Job Ndugai kumvua nafasi yake ya ubunge.
Akisoma maamuzi hayo Jaji wa Mahakama hiyo Latifa Mansoor, amesema maombi ya mbunge huyo yameondolewa kutokana na uamuzi ambao umetolewa siyo wa spika ndugai binafsi bali ni kanuni za kudumu za bunge ndivyo zinavyoelekeza.
Jaji Mansoor amesema kanuni za kudumu za bunge zinaelekeza wazi kuwa mbunge anakoma kuwa mbunge kutokana na kutohudhuria mikutano ya mbunge kwa muda uliolekezwa hivyo uamuzi ambao umetolewa kutangazwa spika ni kutokana na kanuni zilizopo.
Machi 20 mwaka huu aliyekuwa mbunge wa arumeru mashariki aliwasilisha maombi mahakama kuu kanda ya Dodoma ya kufungua kesi ya msingi kupinga uamuzi wa spika kumvua ubunge kwa kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list