We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, February 26, 2019

Wabunge CCM wapashana mbele ya Makamu wa Rais


Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan jana Jumatatu Februari 25, 2019 alimaliza ziara yake mkoani Tabora kwa kubaini kuwapo mgogoro na maneno ya chini kwa chini miongoni mwa baadhi ya wananchi na viongozi.

Akizungumza kwenye mkutano wa  hadhara wa mwisho mjini Tabora, Samia alisema mwanzo wa ngoma ni 'lele' na amebaini kuna zogo linataka kuchomoza.
Akizungumza taratibu alisema tabia hiyo sio nzuri na hataki kuwaficha kwani kiongozi mmoja anasema jambo kuwa wana Tabora wana majungu na mwingine anajibu kuwa ni wakarimu.
Makamu wa Rais alikuwa akiwazungumzia wabunge wa CCM, Emmanuel Mwakasaka (Tabora Mjini) na Munde Tambwe (Viti Maalum) ambao walipopewa nafasi ya kuzungumza na mkuu wa mkoa, Aggrey Mwanri ni kama walijibizana.
Mwakasaka alipopanda jukwaani alisema wana Tabora wana majungu kwani viongozi wengi wanapofanya kazi wanakuwa wanatuhumiwa na kutaka tuhuma zao zifanyiwe kazi kwa undani.
Mbunge huyo alifikia kumtaja kiongozi mmoja wa dini kuwa aliwahi kusema kama wanatafutwa viongozi wa majungu basi katibu atatoka Kigoma na mwenyekiti wake Tabora.
Mbunge Munde naye alipopanda jukwaani alisema Tabora sio wanafiki na kwamba ni wakarimu na pia wanasema ukweli,
Alisema kama kuna changamoto ni za watu wachache na kwamba kukwaruzana hakukosi kwani  kupo kila sehemu.
Munde ambaye alieleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano, alisema changamoto mbalimbali zinazowakabili wakazi wa manispaa ya Tabora na kisha kujibu madai ya mbunge mwenzake Mwakasaka kabla ya kueleza kuwa atamuunga mkuu wa wilaya, Eric Komanya katika kampeni yake ya ujenzi wa madarasa kwa kuahidi kuchangia saruji mifuko 100.
Akielezea hali hiyo, Samia alisema yeye asingesema kama majibizano hayo yasingekuwapo na kuwataka wana Tabora waachane na vimaneno na kama mtu hafai waseme.
"Sisi watu wa pwani tuna msemo wa mwanzo wa ngoma ni lele na hapa naiona lele," alisema.
Alisema amebaini kuna tatizo baada ya kusikia majibizano hayo kwa mmoja kueleza jambo na mwingine kulijibu.
Makamu huyo wa Rais alisema amesikia kuna mabango na kuwataka walio nayo kuyainua juu akisisitiza kutoelewana huko hakutaufikisha mkoa mbali kimaendeleo
Akimzungumzia mkuu wa wilaya, alisema kuwa ni kijana mdogo na kama ana kasoro basi akalishwe kitako na kasoro zake aelezwe ili ajirekebishe.
Akionyesha kukerwa na jambo hilo, Makamu wa Rais alitaka mambo hayo yarekebishwe.
Wakizungumzia suala hilo, baadhi ya wananchi walieleza kufurahishwa na Makamu wa Rais kuwa muwazi katika jambo hilo wakisema litaweka mambo vizuri.
"Unajua sio siri hawa waheshimiwa kuna mkwaruzano ambao umeachwa pasipo kushughulikiwa na ndio maana wamejibizana hadharani," alisema Simon Jerome mkazi wa Isevya.
Mmoja wa  viongozi ndani ya CCM ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema mkwaruzano uliopo ni wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka kesho.
"Wote watagombea ubunge hilo halina shaka na ndio chanzo cha mtafaruku huu wote tulioushuhudia leo (jana)," alisema.
Makamu wa Rais alimaliza ziara yake akiwashukuru wananchi na viongozi wa mkoa huo kwa mapokezi mazuri huku akipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri baada ya kutembelea wilaya zote saba za mkoa wa Tabora.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list