We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, February 26, 2019

Tetesi za usajili barani Ulaya jumanne hii, Sarri, Kepa, Leicester, Rodgers, Arsenal, na wengine sokoni

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri alimgombeza kipa Kepa Arrizabalaga kwa kupuuza amri yake ya kumtaka kutoka uwanjani wakati wa finali ya kombe la Carabao. (Sun) Kisa hicho kiliwafanya wachezaji wengi wa Chelsea kumkasirikia kipa huyo wa miaka 24 raia wa Uhispania. (Daily Express)



Leicester City imeongeza juhudi za kumuajiri Brendan Rodgers kutoka Celtic kama meneja wao mpya. (Guardian)
Leicester pia inatathmini uwezekano wa kumuajiri meneja wa muda kuchukua nafasi ya Claude Puel hadi mwisho wa msimu huu. (Leicester Mercury)



Manchester United na Chelsea wanamnyatia nahodha wa AC Milan Alessio Romagnoli. Lakini huenda wakakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mabingwa wa Serie A, Juventus. (Calciomercato, via Manchester Evening News)
Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani huenda akalazimika kuuza klabu hiyo endapo itashindwa kupanda ngazi ya kushiriki ligi ya primia. (Daily Mail)
Meneja wa Burnley Sean Dyche, amepuuzilia mbali tetesi kuwa analengwa na Leicester. (Burnley Express)
Arsenal inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumuwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka,21, na iko tayari kufikia bei ya euro milioni 40 iliyoitishwa na klabu yake. (Sun). (Sun)



Nahodha wa zamani wa Manchester United Gary Neville anasema kuwa kutakuwa na ”uasi” Old Trafford ikiwa klabu hiyo haitamuajiri Ole Gunnar Solksjaer kama meneja wake wa kudumu. (Daily Mirror)
Chelsea inajiandaa kumuuza muingereza Kasey Palmer kwa euro milioni nne, licha ya mchezaji huyo wa miaka 22 kutoshiriki mechi ya wakubwa, huku Bristol City ikitafakari kubadili mkataba wake wa mkopo na kuufanya wa kudumu. (Sun)



Meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Peter Stoger, ambaye amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Ujerumani mwezi Mei mwaka jana, anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo kwa mkataba wa kudumu. (Leicester Mercury)
Chanzo BBC.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list