We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, February 25, 2019

Tetesi za usajili barani Ulaya jumatatu hii, Rodgers, Neymar, Mbappe, Ivan Rakitic, Hazard na wengine sokoni

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amesisitiza kuwa klabu hiyo haitamuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, na Kylian Mbappe mwaka huu (Marca) Manchester United imehusishwa na usajili wa kiungo wakati wa Ureno Bruno Fernandes, 24. (A Bola, via Mail)



Meneja wa zamani wa Everton na Manchester United David Moyes amekiri kuwa anawania nafasi ya umeneja wa Leicester iliyoachwa wazi. (BeINSports, via Liverpool Echo)
Arsenal inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumuwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka,21, na iko tayari kufikia bei ya euro milioni 40m iliyoitishwa na klabu yake. (Sun)
Leicester City iko tayari kuilipa Celtic euro milioni sita kumnunua Brendan Rodgers kama meneja wao mpya baada ya kumfuta kazi Claude Puel siku ya Jumapili. (Sun)



Meneja wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho anaamini kuwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Eden Hazard atafanya vyema Real Madrid endapo ataamua kuhamia klabu hiyo ya Uhispania. (London Evening Standard)
Mourinho ana panga kurejea kazini msimu huu. (ESPN)



Arsenal huenda isimpate Marc Overmars kama mkurugenzi wa kiufundi kwasababu Ajax amekataa kumuachilia na haiko tayari kulipwa ofa yoyote, kwa mujibu wa ripoti. (Sun)
Kipa wa Burnley na Uingereza Joe Hart, 31, huenda akahamia katika ligi ya MLS. (Sun)CM
Manchester United na Bayern Munich wanamfuatilia kiungo wa kati wa Croatia na Barcelona Ivan Rakitic, 30. (Mundo Deportivo)
Rakitic amesema kuwa kuwa anataka kusalia Nou Camp baada ya kuulizwa maswali mingi kuhusu kuondoka kwake.. (Marca)



Chanzo BBC.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list