Kocha mkuu wa club ya Dar es Salaam Young Africans Mwinyi Zahera ametangaza kumpa mapumziko mshambuliaji wake wa kimataifa raia wa Burundi Amissi Tambwe kufuatia jeraha la kupasuka usoni.
Mwinyi Zahera ambaye kikosi chake baada ya kumaliza mchezo wa ASFC dhidi ya Biashara United kimeelekeza nguvu zake katika michezo ya Ligi Kuu hususani mchezo wake wa Tanga weekend hii, ameamua kumpumzika Amissi Tambwe baada ya kushonwa nyuzi tano.
Tambwe baada ya kuumia katika mchezo wa jana uliyomalizika kwa sare ya 2-2 ila Yanga kusonga mbele kwa ushindi wa penati 5-4, leo hajafanya mazoezi na wenzake ili aweze kupata muda wa kupumzika, Tambwe aliumia wakati wa mchezo dhidi ya Biashara United baada ya kugongana na golikipa wa Biashara United Nurdin Abarora.
No comments:
Post a Comment