Mbunge wa Wingwi (CUF), Kombo Juma Hamad amesema Rais John Magufuli anapaswa kumuondoa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Ramadhan Kailima kwa madai ya kuhusika katika ubadhirifu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wakati huo akiwa mtumishi.
Akizungumza leo Ijumaa Februari Mosi, 2019 katika mjadala wa taarifa ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2017 bungeni jijini Dodoma, Kombo amesema kati ya watumishi 66 wa halmashauri hiyo ni watumishi wawili tu ndio wamechukuliwa hatua kwa ubadhirifu huo wa Sh3.5bilioni
“Najiuliza huo utakatifu wa Serikali uko wapi? Unaozungumzwa tena na wabunge wa CCM uko wapi? Tuishauri Serikali ichukulie hatua kwa watumishi waliohusika na ubadhirifu huu,” amesema akirejea taarifa hiyo la Laac iliyomtaja Kailima.
Amesema kama Sh3.5bilioni zimepigwa halafu mtumishi aliyekuwepo katika wilaya hiyo kipindi hicho aliteuliwa kuwa
kuwa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwamba licha ya jambo hilo, bado wabunge wa chama tawala wanajisifu kuwa kuna watendaji wanatumbuliwa.
“Halafu tunakuja hapa tunajisifu anatumbua. Tuone leo kwa ripoti hii ambayo imemtaja mkurugenzi (Naibu Katibu Mkuu sasa) huyu ambaye anaitwa Ramadhan Kailima leo akamtumbue,” amesema.

No comments:
Post a Comment