Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewatoa wasiwasi Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuwa hana mpango wa kuondoka Yanga
Tangu jana zilisambaa taarifa za Zahera kujiunga na Azam Fc, mtandao wa EATV ukiripoti kuwa kocha huyo atatangazwa kuwa kocha Mkuu wa Azam Fc wakati wowote
"Taarifa hizo hazina ukweli wowote, mimi nina mkataba na Yanga," amesema Zahera
"Hakuna mazungumzo yaliyofanyika kati yangu na Azam Fc. Siwafahamu viongozi wa Azam sijawahi kukutana nao mahali popote"
"Nawaambia Wana Yanga wapuuze taarifa hizo. Pia nawaambia wapuuze uzushi mwingi unaoenezwa juu yangu. Jambo lolote likitokea nitawataarifu mimi mwenyewe. Hata kama nikisafiri kwenda Congo nitawaambia"
Taarifa ya Zahera kutimkia Azam Fc imestua mashabiki wa Yanga hasa ikizingatiwa kocha huyo amekuwa chachu ya mafanikio ya kikosi cha Yanga msimu huu
Jana Azam Fc iliwafuta kazi kocha Hans van Pluijm na Msaidizi wake Juma Mwambusi na sasa inasaka warithi wa nafasi hizo
No comments:
Post a Comment