Mwanaume na mwanamke wanahitajiana. Kila mmoja anamhitaji mwenzake. Mume hawezi kukamilika bila mke na mke hawezi kukamilika bila mume. Mwanamke ni vazi la mwanaume na mwanaume ni vazi la mwanamke. Wote wanakamilishana.
Katika maisha ya mwanaume kuna picha ya mwanamke ambayo huwa haifutiki kwa kumuona kuwa anayakamilisha maisha yake. Mwanamke ambaye huwa ni kama vazi zito wakati wa msimu wa baridi, na kama vazi maridhawa wakati wa msimu wa joto.
Humuona hivyo kutokana na sifa alizobeba, sifa zinazomfanya kuwa mkamilishaji wa ombwe linalojitokeza katika maisha yake.
Ungana nami katika kuzisawiri sifa hizo za mwanamke ambaye picha yake haiwezi kuondoka katika akili yake:
- MWANAMKE ANAYEUVAA UHUSIKA WA KIKE:
Huyu ni yule anayemfanya mumewe kuwa mwanaume. Kadiri anavyovaa uhusika wake wa kike ndivyo mume anavyozidi kuhisi uanaume wake.
Mwanamke huyo huuvaa uhusika wake wa kike bila hata kuongea wala kuuonesha kwa mavazi, mwanaume anauhisi moja kwa moja. Ni uhusika wa kike wa kweli na wa ndani ambao mwanaume hauoni kwa macho bali anauhisi… Huyo ni mwanamke ambaye mwanaume hatomsahau.
- MWANAMKE MBEMBEZI:
Huyu ni yule anayeutambua uhalisia wa mwanaume husika, akaingia katika maisha yake na kushirikiana naye katika kila jambo, liwe la kuhuzunisha au la kufurahisha… Ni mwanamke anayeshirikiana naye hata kwa mawazo yake…
Huyo sio yule anayekuwa mtazamaji tu wa matukio yanayomtokea mwanaume, bali huyaishi matukio hayo kwa moyo wote huku akimpa hamasa, kumshajiisha na kumtengeneza kuwa mshindi dhidi ya matukio hayo.
- MVUMILIVU:
Mwanaume hawezi kumsahau mwanamke aliyevumilia na kustahmili changamoto na mashinikizo mbalimbali.
Mwanamke ambaye hampi shinikizo, ambaye anajua cha kuongea kwa upendo na upole, anayostahmili hata silika zake na kuamiliana naye kwa hekma, ni ngumu mno kwa mwanaume kumsahau mwanamke huyo… Hakika anaweza kubaki katika kumbukumbu zake daima dawamu.
- MWANAMKE ROMANTIC:
Mwanaume anapenda aishi na mwanamke mwenye kumfanya ahisi utamu muda wote. Mwanamke mwenye umaridadi wa kike, anayemfanya asahau shida zote za dunia. Huyo ni vigumu kumsahau.
- MWANAMKE MWEREVU:
Huyu ni mwanamke anayejua NAMNA ya kuamiliana na mumewe, anajua kuwa kila mwanaume ana silika zake maalum, anajua wakati wa kuzungumza naye, anajua wakati na namna ya kumuomba jambo, anajua wakati gani wa kukaa kimya na kumsikiliza.
Mwanamke huyo anajua jinsi ya kumfanya mumewe achomoze na kusonga mbele kwa sababu muda wote anamfanya ajiamini na kuipa nguvu shakhsia (personality) yake.
Mwanaume hawezi kumsahau mwanamke wa aina hiyo kwa sababu humuona kuwa mshirika halisi wa mafanikio yake, na anapokuwa karibu naye anakuwa muwazi zaidi.
- MWANAMKE MARIDHAWA:
Mwanaume hawezi kumsahau mwanamke maridhawa, mwenye utuvu wa ndani, aliyetulia.
Huyu ni mwanamke ambaye uzuri wake ameufanya kuwa maalum kwa ajili ya mumewe tu, mwanamke anayempa utulivu mumewe katikati ya zahma za maisha… Mwanamke ambaye mume huona raha kurudi nyumbani badala ya kuona karaha.
- MWANAMKE MSAMEHEVU:
Mwanaume anampenda mwanamke mwenye mtazamo chanya, mwenye mawazo chanya na mwenye fikra chanya ambaye humfanya mume kuhisi kuwa maisha yake ni kama kitabu kilichofunguliwa.
Hakika mwanamke ambaye hana kusubiri makosa ya mumewe na kumnanga, huyo ni mwanamke ambaye hawezi kusahaulika katika maisha yake.
- MWENYE UPENDO KAYAYA:
Huyu ni mwanamke mwenye hisia za upendo wa hali ya juu ambapo huweza kumzamisha mumewe katika bahari ya upendo kiasi kwamba anapokuwa pamoja naye sio tu kwamba anahisia kuwa yuko pamoja na mke na kipenzi, bali wakati mwingine huhisi kuwa anaakisi upendo wa mama yake. Mwanaume ni kama mtoto mkubwa lakini tofauti ni kwamba mahitaji ya mtoto huyu mkubwa ni zaidi ya mahitaji ya mtoto mdogo. Daima humtarajia mkewe amzamishe kikamilifu katika bahari ya upendo na mahbba.
- MWENYE KUJITOA:
Mwanamke huyu huacha athari isiyosahaulika katika maisha ya mwanaume. Daima huuhisi uwepo wake na kwamba yuko tayari kutoa chochote alichonacho kwa ajili ya mumewe bila kutarajia mrejesho na bila vikwazo, kwani mwanaume anamchukia mwanamke ambaye hutoa kile alichonacho ili kumuweka kwenye kifungo cha moyo na maisha.
- MWANAMKE IMARA MWENYE KUJISHUSHA:
Mume anapenda mke ajue ni wakati gani anatakiwa kuwa ngangari na wakati gani anatakiwa kushuka. Humpenda mke ambaye ni imara lakini anayemfanya auhisi uanaume wake. Hampendi yule ambaye muda wote anaonekana ni mnyonge kwa sababu hilo litaonesha picha isiyokuwa maridhawa

No comments:
Post a Comment