Jina la mwimbaji Davido linazidi kutawala duniani na safari hii ataungana na wakali kama Cardi B, Future, Tory Lane, Migos na wengine kibao kutumbuiza kwenye stage moja katika tamasha la VestVille ambalo litafanyikaUbelgiji mwishoni mwa February,2019.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Davidoamegusia kuhusu tamasha hilo ambalo litawakilisha wasanii kibao na kuandika ujumbe unaosema “Festival Season 2019, Viwango vya juu vimefunguka”
January 28,2019 Davido alishika nafasi ya pili kwa ujumla kuujaza uwanja wa O2 mjini London Uingereza baada ya Wizkid na amevunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza mwenye umri mdogo kutokea katika Bara la Afrika kuujaza uwanja huo.
No comments:
Post a Comment