We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, January 31, 2019

HAYA HAPA MATOKEO YA YANGA VS BIASHARA UNITED LEO


Yanga imetinga raundi ya tano ya michuano ya kombe la FA (ASFC) baada ya kuifunga Biashara United kwa mikwaju ya penati 5-4 kufuatia matokeo ya sare ya mabao 2-2
Mchezo huo ulianza kwa kasi ambapo makosa ya beki Andrew Vicent Chikupe aliyemfanyia madhambi mshambuliaji wa Biashara United ndani ya eneo la hatari, yaliizawadia timu hiyo mkwaju wa penati uliowekwa kambani mapema tu na Waziri Junior

Yanga ilirejea mchezoni kwenye dakika ya tisa ikipata mkwaju wa penati baada ya Ajib kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
Mkongwe Amissi Tambwe akautumbukiza mpira kimiani

Kwa mara nyingine tena Biashara United wakafunga bao la pili kwenye dakika ya 40 kupitia kwa Innocent Edwin aliyewaramba chenga walinzi wa Yanga kabla ya kuutumbukiza mpira kimiani

Yanga ilirejea ikiwa imara kwenye kipindi cha pili ikisaka bao la kusawazisha.
Baada ya kosakosa nyingi, Makambo aliisawazishia Yanga bao la pili kwenye dakika ya 74 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango wa Biashara United, Barola
Baada ya dakika 90 kukamilika huku timu hizo zikitoka sare ya mabao 2-2, mshindi wa mchezo huo ikabidi aamuliwe kwa changamoto ya mikwaju ya penati

Yanga ilifanikiwa kufunga penati zake zote tano wakati Tarik Mussa alikosa mkwaju mmoja wa Biashara United.

Yanga sasa itachuana na Namungo Fc kwenye mchezo wa raundi ya tano

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list