Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema ameridhishwa na mazoezi ya kwanza ya kikosi chake yaliyofanyika jana nchini Misri kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly
Licha ya hali ya baridi kali, Aussems amesema wachezaji wake wamekuwa na mwitikio mzuri yapo matumaini makubwa ya timu hiyo kufanya vizuri katika mchezo wa keshokutwa
Pia Aussems amethibitisha nahodha wa Simba John Bocco yuko timamu kabisa kiafya na anatarajia kumtumia kwenye mchezo utakaopigwa Jumamosi, Feb 02 2019 saa nne usiku wa saa za Tanzania
"Nimeridhishwa na mazoezi tuliyofanya mchana wa leo," amesema Aussems
"Yalikuwa ni mazoezi maalum ya kuelekezana nini tunatakiwa kufanya na kipi tukiepuke katika mchezo huo"
"Hali ya hewa hapa ni baridi kali lakini nimefurahishwa mwitikio wa wachezaji katika mazoezi tunayofanya"
"Bocco amerejea, ni moja ya silaha ambazo natarajia kuzitumia kwenye mchezo wa keshokutwa"
No comments:
Post a Comment