Kocha wa zamani wa Arenal, Arsenal Arsene Wenger yupo kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa na miamba ya Italia AC Milan kurithi mikoba ya kocha Marco Giampaolo. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, anatarajiwa kukataa ofay a kuchezea timu ya taifa ya Nigeria na badala yake kuelekeza nguvu zote kwa England iwapo ataitwa na kocha Gareth Southgate katika michezo ya kufuzu Euro 2020 dhidi ya Jamhuri ya Czech na Bulgaria. (Telegraph)
Mkurugunzi wa michezo wa Borussia Dortmund amefichua kuwa hadhani kuwa nyota wao kinda Jadon Sancho, 19, akisalia klabuni hapo kwa muda mrefu. Sancho kutoka England alikuwa akihusishwa na Man United katika dirisha la usajili lililopita. (Kicker, via Mail)
Beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Ivory Coast Eric Bailly sasa kusalia nje ya uwanja mpaka mwezi Januari. Baily, 25, alipata majeraha ya goti kwenye mchezo wa kujiandaa na msimu dhidi ya Tottenham. (Sun)
Beki wa Tottenham Jan Vertonghen, 32, ambaye makataba wake unaisha mwishoni mwa msimu amesema kuwa anaweza kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (London Evening Standard)
Spurs tayari wameshafungua mazungumzo na Mbelgiji huyo Vertonghen, ili kumuongezea mkataba. (Mail)
Mchezaji wa Juventus anayewindwa na Manchester United Mario Mandzukic, 33, pia anawaniwa na klabu ya ligi kuu nchini Marekani Angeles FC. (Calciomercato - in Italian)
Manchester United wanahusishwa na kutaka kumsajili beki wa Tottenham na timu ya taifa ya Ubelgiji Toby Alderweireld, 30, katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. (Tuttosport, via Inside Futbol)
Arsenal wanapanga kumfuatilia kinda wa klabu ya RB Salzburg Dominik Szoboszlai, 18, kwenye mchezo dhidi ya Liverpool wiki hii. Arsenal wanatarajiwa kutuma ofay a kumnasa kinda huyo mwezi Januari. (Football Insider)
Juventus na Inter wanaweza wakajikuta wakiminyana vikali kwenye dirisha la usajili mwezi Januari kugombea saini ya kiungo wa Brcelona na Croatia Ivan Rakitic, 31. (Calciomercato, via Caught Offside)
Klabu ya AS Roma inamfuatilia kwa karibu winga wa Wolves raia wa Uhispania Adama Traore, 23. (Calciomercato)
TUMEBORESHA APP YETU, TAFADHALI BOFYA HAPA CHINI KUDOWNLOAD APP YETU MPYA ILI KUENDELEA KUPOKEA HABARI KWA WAKATI NA KUTAZAMA MECHI ZOTE LIVE ( UKISHA BOFYA, BONYEZA NENO OPEN IN PLAY STORE KISHA INSTALL )
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YETU MPYA BURE KABISA
No comments:
Post a Comment