Pamoja na mashabiki wa Yanga kuwa na matumaini makubwa kwa usajili wa kiungo mshambuliaji Issa Bigirimana, nyota huyo bado hajaanza kuonyesha makali yake kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Bigirimana alitua Yanga akitokea klabu ya APR ya nchini Rwanda, akitua sambamba na Patrick Sibomana aliyekuwa akicheza Mukura Victory
Sibomana ameingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Mwinyi Zahera lakini hali ni tofauti kwa Bigirimana ambaye amecheza mechi chache kwa dakika chache
Zahera ametaja sababu ya nyota huyo kuchelewa 'kushika kasi' kuwa ni ugeni wake kwa soka la Tanzania
Zahera amesema Bigirimana bado hayuko fit, atahitaji muda zaidi ili kuweza kwenda sambamba na wenzie
Kiungo huyo aliyepachikwa jina la utani 'Walcott', aliwahi kubainisha kuwa mazoezi ya Tanzania ni magumu kulinganisha na mazoezi waliyokuwa wakifanya Rwanda
"Hapa mazoezi ni magumu sana, ni tofauti na kule kwetu Rwanda. Tunafanya mazoezi ya kukimbia siku tatu tu halafu tunacheza mpira lakini hapa tunakimbia kila siku," alisema
Aidha Zahera amesema kiungo huyo pia alipata majeraha ya nyama za paja ambayo yamemrudisha nyuma lakini anaamini baada ya muda mchango wake utaonekana Yanga
No comments:
Post a Comment