Kampuni ya Google' ambao ni wamiliki wa mtandao wa YouTube wametozwa faini ya zaidi ya TZS bilioni 344 baada ya kukiuka sheria ya usimamizi wa faragha kwa watoto nchini Marekani.
Inaelezwa kuwa YouTube walikiuka sheria ya faragha nchini Marekani, ambayo inakataza usambazaji wa taarifa zinazohusu watoto walio chini ya miaka 13 bila kuwa na usimamizi wa wazazi.
YouTube inashika nafasi ya pili juu ya Google kwa mujibu wa (Alexa.com) kuwa na watembeleaji wengi zaidi, imekuwa ikilalamikiwa na watu kuhusu ukiukaji wa faragha hususani za watoto hasa kutokana na kuruhusu machapisho ya video kusambaa bila kuwa na usimamizi wa wazazi.
Ili kupunguza tuhuma hizo mwaka 2015 YouTube walianzisha App maalum kwaajili ya watoto lakini bado kumekuwa na changamoto kutokana na kukosa watumiaji wengi kama App mama ya ambayo kwa mwezi inapata watembeleaji hai zaidi ya bilioni 2.
No comments:
Post a Comment