Dk David Luhago anatajwa kuchukua nafasi ya Katibu Mkuu wa Yanga, akipitishwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji jana
Taarifa za kuaminika zimebainisha pia kuwa Mwanahabari Hassan Bumbuli amepitishwa kuwa Afisa habari mpya wa Yanga wakati Antonio Nugaz amepitishwa kuwa Afisa Uhamasishaji
Hivi karibuni Yanga ilitangaza nafasi hizo kuwa wazi ikisaka watu sahihi
Nafasi ya Katibu Mkuu ilikuwa ikikaimiwa na Dismas Ten ambaye pia ndiye aliyekuwa Afisa Habari
Mtu wa kwanza kushikilia nafasi hiyo alikuwa Omary Kaya aliyekabidhiwa baada ya Charles Mkwasa kujiuzulu

No comments:
Post a Comment