We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, September 14, 2019

Yanga leo inaweza kuwa hivi mechi dhidi ya ZESCO

Langoni kocha Mwinyi Zahera atahitaji kufanya uamuzi kama aendelee na Metacha Mnata au amuanzishe Farouk Shikalo ambaye leseni yake kutoka CAF imewasili
Mapinduzi Balama anaweza kuanzia upande wa kulia kuchukua nafasi ya Paulo Godfrey 'Boxer' ambaye majeraha bado yamemuweka nje
Lakini pia Juma Abdul amerejea kikosini baada ya kumaliza msiba wa mama yake mkoani Lindi. Amefanya mazoezi kwa siku mbili hivyo Zahera anaweza kumtumia kutegemeana na utimamu wake wa mwili
Safu ya ulinzi wa kati haitarajiwili kuwa na mabadiliko, Lamine Moro na Kelvin Yondani watakuwa na jukumu la kuwadhibiti washambuliaji wa ZESCO wakiongozwa na Mkenya Jesse Were
Ally Mtoni nae huenda akaendelea kutunza nafasi yake ya ulinzi wa kushoto
Upande wa kiungo nahodha Papy Tshishimbi ataendelea kuiongoza timu, Mohammed Issa 'Banka' na Feisal Salum/Makame wanaweza kuanza pamoja leo kama Zahera ataamua kutumia viungo watatu lakini kama sivyo huenda Banka akaanza na pengine Ngasa akacheza winga ya kulia iwapo Balama atarudishwa namba mbili
Safu ya ushambuliaji kama kawaida itaongozwa na Patrick Sibomana, Juma Balinya na Sadney Urikhob
Yanga leo inahitaji kushinda hivyo ni dhahiri Zahera atatumia mbinu itakayompa uwezo wa kushambulia kwa nguvu timu inapokuwa na mpira na pia kuwa imara kwenye ulinzi

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list