We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, September 14, 2019

Waziri akanusha taarifa za ugonjwa wa Ebola

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu, ametoa tahadhari na kuwataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na kudhibiti ili ugonjwa wa Ebola usiingie hapa nchini.
Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Septemba 14 wakati akitoa taarifa za uvumi wa uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini na kuwatoa  hofu wananchi kuwa hakuna dalili za ugonjwa huo kuwepo licha ya kuripotiwa katika nchi jirani.
''Naomba niwatoe hofu wananchi, hadi sasa hakuna mgonjwa yoyote wa Ebola aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo'', amesema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amezitaja dalili za ugonjwa wa Ebola ambazo ni homa kali, kuumwa kichwa, kutapika na kuharisha, viungo vya mwili kuuma pamoja na  kutokwa damu katika matundu yote ya mwili.
Waziri Ummy ameongeza kuwa licha ya watanzania kuwa na utamaduni wa kupeana mikono ni vyema ukawekewa tahadhari ya kunawa mikono mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list