We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, September 26, 2019

Waziri Mkuchika Azitaka Taasisi Zilizo Chini Ya Ofisi Ya Rais Kuwa Mfano Wa Kuigwa Kiutendaji Na Kimaadili

Na James K. Mwanamyoto
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika amewataka watumishi wa taasisi za umma zilizo chini ya Ofisi ya Rais kuwa mfano wa kuigwa na watumishi wa taasisi nyingine za umma kiutendaji na kimaadili kwa kuwa jamii inaitazama Ofisi ya Rais kama kioo cha utendaji kazi mzuri katika utumishi wa umma.

Waziri Mkuchika ametoa wito huo wakati wa kikao kazi chake na Watumishi Waandamizi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa chuo hicho.

Mhe. Mkuchika amewaasa watumishi wa taasisi hizo kujiona kuwa ni sehemu ya kuitunza heshima ya Ofisi ya Rais kwa kufanya kazi kwa uadilifu.

Amewasisitiza watumishi wa chuo hicho kufanya kazi kwa bidii, umoja na mshikamano ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kuharakisha maendeleo ya nchi.

“Mimi nipo kwa ajili ya kumsaidia Mhe. Rais ambaye ndiye Waziri wa Ofisi hii kusimamia utendaji kazi wa taasisi zote zilizopo chini ya ofisi yake, hivyo hatuna budi kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi kama ambavyo yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele kutekeleza majukumu yake kwa vitendo”, amesisitiza Mhe. Mkuchika.

Aidha, Mhe. Mkuchika ametoa rai kwa Watumishi wa Umma wote nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni, Sheria, Taratibu na Miongozo ya kiutumishi iliyopo ili kuepukana na vitendo vya ubaguzi wa kijinsia, dini, ukabila na  itikadi za kisiasa kwa wananchi na watumishi wenzao wanaowahudumia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel S. Shindika kwa niaba ya chuo, amemthibitishia Mhe. Mkuchika kuwa, atahakikisha maelekezo yote aliyoyatoa yanatekelezwa ili kuendana na kasi ya kiutendaji ya Mheshimiwa Rais yenye lengo la kuleta maendeleo ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list