We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, September 13, 2019

Walimu 10 mbaroni kwa wizi wa mitihani

Mara baada ya Mtihani wa Darasa la Saba kumalizika siku ya Alhamisi ya Septemba 12, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, limetoa taarifa ya uwepo wa udanganyifu wa mtihani huo kwa baadhi ya shule za mkoani humo.

Akizungumza leo Septemba 13, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoani humo ACP Revocatus Malimi, amesema kuwa hadi sasa jeshi hilo,  linawashikilia Walimu 10  kwa tuhuma za wizi wa mitihani katika Shule ya Msingi Kumunazi Wilayani Ngara.
Kamanda Malimi amesema kuwa,Walimu hao walikutwa wamejifungia kwenye nyumba ya mmoja wa walimu, huku wakiandaa majibu ya somo la Sayansi, tukio ambalo linawajumuisha Walimu wa Shule hiyo pamoja na Walimu wasimamizi, walioteuliwa kusimamia mtihani huo.
''Kitendo kilichofanywa na watuhumiwa hao ni kosa la jinai kwani, mitihani mbali kuwa ni kipimo cha kuwaandaa na kuwapata wataalamu wa baada ni siri kuu  ya nchi, licha ya kupewa semina na kula kiapo cha uadilifu ikithibitika wamehusika na udanganyifu wa aina yoyote wakifikishwa mahakamani adhabu yake  ni  kubwa'' amesema ACP Malimi.
Aidha Kamanda Malimi amesema, bado wanaendelea na upelelezi na pindi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list