Jurgen Klopp wa Liverpool, Pep Guardiola wa Manchester City na Mauricio Pochettino kutoka Tottenham ni miongoni mwa walimu watatu waliyotajwa kuwania tuzo ya kocha bora wa FIFA.
Habari hizo zimeanza kuenea asubuhi ya leo siku ya Jumatatu kufuatia kuwa na msimu mzuri wa mwaka 2018/19 kwa makocha hao.
Kwa upande wake Klopp alifanikiwa kunyakuwa taji la Champions League akiwa na Liverpool kwa kumfunga Tottenham katika jiji la Madrid baada ya Mauricio Pochettino kuifikisha Spurs katika hatua hiyo ya fainali kwa mara yake ya kwanza.
Wakati kwa upande wa Guardiola ameiyongoza City kunyakuwa taji la Premier League mara mbili mfululizo baada ya kuizidi Liverpool after kwa kujivunia point 98.
Huku makocha hawa wawili Guardiola na Klopp wakitarajiwa kuzidi kupambana msimu huu kuwania taji hilo la Premier League.
Man City na Liverpool pia wamewakilishwa katika kundi la magoli kipa bora, Ederson na Alisson sambamba na Barcelona, Marc-Andre Ter Stegen kwenye listi hiyo.
Liverpool imemuingiza pia mchezaji wake Virgil van Dijk akishindana na Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo katika kuwania kipengele cha uchezaji bora, inakumbukwa pia beki huyo aliwashinda nyota hao kwenye tuzo ya ‘UEFA Player of the Year’.
No comments:
Post a Comment