We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, September 18, 2019

VIDEO: Agizo la PM Majaliwa baada ya wananchi kukodi gari la wagonjwa kwa laki 8

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupeleka gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya cha Kibaoni kilichopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara ili kuwapunguzia wananchi gharama ya kukodi gari kwa Tsh. Laki 8 pale wagonjwa wao wanapopata rufaa.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumanne, September 17, 2019 wakati akizungumza na Wananchi wa Mji wa Ifakara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa kituo cha mabasi cha mji huo ambapo amesema iwapo fedha za makusanyo ya mapato ya ndani  katika Halmashauri husika zingekuwa zinatumika vizuri kusingekuwa na changamoto  kama hizo.
Kauli hiyo imekuja kufuatia Wananchi wa Mji wa Ifakara kuiomba  Serikali iwasaidie kuwapatia gari la wagonjwa kwani kitua chao hakina gari na wagonjwa wao wanapopata rufaa ya kwenda hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro wanalazimika kukodi gari kutoka hospitali ya Mtakatifu Francis kwa gharama ya Tsh. 800,000 ambazo baadhi yao wanashindwa kuzimudu.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list