Si wanawake pekee ambao huwa bize kuona wanakuwa na maumbile mazuri na kwamba wanakuwa ni wenye kuvutia muda wote.
Wapo wanaume wachache sana ambao wamebarikiwa kuwa na uume mkubwa kwa asili. Aina ya maisha unayoamua kuishi yanaweza kuathiri ukubwa na uimara wa uume wako.
Kwahiyo ikiwa una shaka kidogo juu ya ukubwa wa uume wako usihofu zifuatavyo ni vipimo vitavyo kutibitishia kua uume wako ni sahihi kabisa.
Mwanamke yeye huwa na uke wenye urefu wa inch 4 ingawa unaweza kuongezeka ukubwa kutegemea na namna anavyoandaliwa au mwanaume mwenyewe alivyo.
Kwa watu wazima, wastani wa ukubwa wa uume uliosimama ni kati ya inch 3.9 mpaka 5.8 (9.9-15 cm). Wapo pia wanaume wachache ambao kwa asili wana uume wa ukubwa wa inch 7 au 8.
Uume unachukuliwa kuwa mdogo ikiwa uko chini ya inch 4 (chini ya sentimita 10) ukiwa umesimama. Usiwaze ukubwa wa uume ukiwa umelala.
Kuna wanaume wa aina mbili, kuna wale ambao uume ukiwa umelala huonekana ni mkubwa lakini uume utakaposimama hauwi mkubwa sana na kuna wale ambao uume ukiwa umelala uume wao unaonekana ni mdogo sana na ndiyo hao ukisimama unakuwa mkubwa zaidi hata ya wale ambao ukiwa umelala unaonekana ni mkubwa.
Hivyo ukiona uume wako umelala na unaonekana ni mdogo sana usiwaze, ni hali ya kawaida, unatakiwa uwaze ukiwa umesimama kabisa.
No comments:
Post a Comment