Baada ya club ya Azam FC kupoteza kwa mara ya kwanza katika uwanja wake wa nyumbani katika mechi za kimataifa toka waanze kuutumia, kwa kufungwa 1-0 na Triangle FC ya Zimbabwe katika mchezo wa Kombe la shirikisho.
Azam FC baada ya kupoteza mchezo huo katika uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi, leo walikuwa Bulawayo Zimbabwe kucheza mchezo wa marudiano ili kupambania nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho.
Game iliendelea kuwa ngumu kwa Azam FC baada ya kujikuta wakiondolewa tena kwa kufungwa 1-0, hivyo wameaga michuano hiyo kwa kufungwa jumla ya magoli (aggregate 2-0), Azam FC sasa wanarudi nyumbani kushindana katika michezo ya Ligi Kuu na Kombe la FA (ASFC).
No comments:
Post a Comment