Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanzania Bara (TLS) limezitaka mamlaka zilizopewa nguvu ya kuwachukulia hatua mawakili kuwasikiliza kabla ya kuwachukulia hatua.
Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa jana Septemba 26, 2019 imesema “Baraza la Uongozi linawataarifu wale waliopewa mamlaka ya kuwaonya na kuwasimamisha mawakili kuwapa haki ya kusikilizwa kabla ya kuwapa adhabu kali ya kusimamishwa au kuondolewa kabisa kwenye uwakili” imesema taarifa ya Baraza hilo iliyosainiwa na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania Bara (TLS), Dk. Rugemeleza Nshalla.
Taarifa hiyo imesema kuwa sheria ya chama hicho inampa mamlaka Jaji Mkuu au Jaji yoyote wa Mahakama Kuu kumuonya au kumsimamisha wakili yoyote lakini kumsimamisha wakili bila kumpa haki ya kusikilizwa ni kivunja sheria.
Baraza la uongozi la TLS limetoa taarifa yake siku Saba baada ya Rais mstaafu wa Chama hicho Fatma Karume kusimamishwa uwakili.
Fatma ambaye ni mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Abeid Aman Karume alisimamishwa uwakili Ijumaa iliyopita ya Septemba 20, 2019 kwa madai ya kuishambulia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na atafikishwa kamati ya maadili ya mawakili kujadiliwa.
No comments:
Post a Comment