Mshambuliaji Sadney Khoutage leo ameweza kuifunga Yanga bao lake la kwanza katika mashindano msimu huu
Sadney alifunga bao la kusawazisha dhidi ya Zesco United baada ya kupokea mpira akiwa ndani ya eneo la hatari katika mchezo ambao Zesco ilishinda kwa mabao 2-1
Sadney amehusika kwenye mabao yote mawili yaliyofungwa na Yanga dhidi ya Zesco katika michezo yote miwili
Ameeleza furaha yake baada ya leo kufanikiwa kufunga, akiishukuru familia na wote waliokuwa wakimuunga mkono kipindi chote
"Nilipoanza kufikiria jinsi nilivyobarikiwa machozi yalianza kunitoka. Namshukuru Mungu, familia na marafiki zangu, afya njema pamoja na nguvu za kupambana"
"Nawapenda wote," aliandika Sadney kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Bao alilofunga leo litamuongezea kujiamini mshambuliaji huyo ambaye alianza maisha yake kwa kusuasua kwenye klabu ya Yanga
Hakuna shaka ataendelea kuwa na mchango mkubwa kwa kikosi cha Yanga kwenye ligi na michuano ya kombe la Shirikisho ambayo Yanga itakuwa ikisaka nafasi ya kutinga makundi
No comments:
Post a Comment