Inadaiwa, Cristiano Ronaldo amekataa kuvaa jezi ambayo inanembo ndogo ya dhahabu maeneo ya kifuani maarufu kama ‘Serie A badge’ ambayo huwekewa wachezaji waliyofanya vizuri msimu uliyomalizika. Sababu zikidaiwa kuwa ni kukwepa fitna ya kuonekana ni bora zaidi ndani ya klabu kuliko wenzake.
Ronaldo amekuwa na msimu mzuri uliyomalizika baada ya kufunga jumla ya mabao 28 huku akichangia pasi 10 za mwisho zilizochangia magoli hao.
Kutokana na kufanya vizuri 2018/19, Cristiano Ronaldo ametajwa kama mchezaji bora wa msimu huo. Kwa mujibu wa gazeti la michezo la Marca, ligi ya Serie A imewapatia ‘badges’ maalum kwa washindi mbalimbali waliyofanya vizuri baada ya kumalizika kwa msimu.
Miongoni mwa waliyopata ‘badges’ hizo ni pamoja na Samir Handanovic (goli kipa bora wa msimu) Nicolo Zaniolo (mchezaji bora kijana), Kalidou Koulibaly (beki bora wa msimu), Sergej Milinkovic-Savic (kiungo bora wa msimu) Fabio Quagliarella (mshambuliaji bora) na Cristiano Ronaldo (mchezaji bora).
Serie A iliiwachia wachezaji wenyewe kuamua kama ‘badges’ hizo ambazo ni kama heshima kwa waliyofanya vizuri kama wangependa kuwa kwenye jezi zao mpya, lakini Ronaldo amekataa kuweka huku ikiripotiwa kama nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, kukwepa kuonekana kama bora zaidi mbele ya wachezaji wenzake wa Juventus.
No comments:
Post a Comment