Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amemwapisha Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), leo Jumanne Septemba 3, 2019, Bungeni jijini Dodoma. Mtaturu amechukua nafasi ya Tundu Lissu ambaye ubunge wake ulifutwa Juni 28, 2018 baada ya kupoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge.
Baada ya Miraji kuapishwa, Spika Ndugai amesema kuwa, sasa watu wa Singida Mashariki wanaye mwakilishi halisi bungeni.
Aidha, wakati Mtaturu akiapishwa asubuhi hii, wabunge wa Upinzani wamesusia tukio hilo kwa kugoma kuingia ukumbini katika kipindi hiki cha asubuhi

No comments:
Post a Comment