We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 17, 2019

Mwinyi Zahera: Yanga itafika makundi hata kama hampendi, aahidi kuwaonyesha wanaobeza kikosi chake

Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amekusudia kuwaziba midomo wanaobeza kikosi chake huku akidai kuwa watawatoa Zesco United, kwenye mchezo wa marudiano wa Klabu bingwa barani Afrika utakachezwa katika jiji la Ndola nchini Zambia.
Related image
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wakicheza nyumbani vijana wa Zahera walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 huku Zesco United FC wakichomoa dakika ya 84 kupitia kwa kiungo wao Thaban Kamusoko.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Spoti Leo online, Kocha huyo raia wa Congo amesema anatambua kwamba watu wengi hawaipi Yanga nafasi ya kutinga hatua ya makundi kutokana na sare hiyo lakini yeye ni kocha mwenye mbinu nyingi zinazomwezesha kupata matokeo na amepania kuwashangaza watu kwa kufanya hivyo Zambia.
“Nataka kuwaonyesha watu hasa wale wanaoidharau Yanga, kwamba tutacheza makundi ya Ligi ya mabingwa kwa kuwatumia wachezaji hawa hawa waliocheza mechi ya kwanza nitaongezea na mbinu zangu mbadala ambazo hatukuzitumia mchezo uliopita nina uhakika tutavuka na midomo wataifunga,” alisema Zahera.
Kocha huyo amesema Zesco siyo timu yakutisha kihivyo kama ambavyo watu wanaizungumzia ndiyo maana baada ya kuwaona na kubaini mbinu wanazotumia amepata uhakika wa kujua cha kufanya na kupata matokeo wakiwa ugenini.
Yanga ili kusonga mbele hatua ya makundi inalazimika kupata sare ya kuanzia mabao 2-2 au ushindi wowote, jambo ambalo litawalazimu kucheza kwa umakini mkubwa sababu Zesco nao wamepania kuendeleza rekodi yao ya kucheza makundi kama wanavyofanya huko nyuma.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list