We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, September 17, 2019

Afariki kwa kuchomwa kisu akidai 1500

Mtu mmoja amefariki dunia kwa kuchomwa kisu baada ya kudai 1500 kama malipo yake.



Mtu huyo aitwaye Rajabu Abdalah amefariki dunia katika tukio hilo lililofanyika Kata ya Babati wilaya ya Babati mkoani Manyara, baada ya mwenzake kumchoma kisu chini ya titi la upande wa kushoto wakiwa wanagombania shilingi 1500.
Imeelezwa kuwa kiasi hicho cha fedha walipewa na abiria kama malipo baada ya kumbebea mzigo wake kuupeleka katika stendi ya magari.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Agustino Senga, amesema kuwa kutokana na opereseheni kubwa iliyofanyika kumsaka kijana Cleophace John a.k.a Mgogo aliyefanya mauaji hayo walifanikiwa kumpata.
''Tumefanya msako mkubwa na kumkamata  mtuhumiwa aitwaye Cleophace John au maarufu Mgogo, akiwa ndani ya gari aina ya Emmigrace leo Asubuhi ya Septemba 17, 2019 akiwa anajaribu kutoroka kuelekea jiji la Dodoma'', ameeleza RPC. 
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mji Mrara, ukisubiri uchunguzi wa daktari, huku mtuhumiwa akiwa mikononi mwa polisi  kwa mahojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list