Hatimaye mwili wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe umezikwa jana Jumamosi, Septemba 28, 2019 kijijini kwake Kutama katika Wilaya ya Zvimba.
Mugabe alifariki dunia Septemba 6, 2019, katika Hospitali ya Gleneagles, nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Jeneza lake lililokuwa na rangi ya shaba lilishushwa kaburini huku likishuhudiwa na waombolezaji wachache ikiwamo familia yake.
Mugabe alikuwa amezungukwa na mkewe Grace, watoto na watu wa karibu wa familia yake. Ni marafiki wachache wa zamani waliohudhuria mazishi hayo.
Alizikwa katika eneo la nyumba ya familia yake. Ni wachache ambao wangedhania mtu mwenye haiba kama yake angezikwa na watu wachache.
Amezikwa mbali na marafiki zake ambao anaamini walimsaliti.
No comments:
Post a Comment