Mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa kati ya Zesco United dhidi ya Yanga utapigwa Jumamosi Septemba 28 2019 saa tisa Alasiri kwa saa za Zambia wakati ambapo huku Tanzania itakuwa saa kumi kamili jioni
Mchezo huo utarushwa mbashara kupitia Azam Sport 2
Yanga tayari iko nchini Zambia ikiendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo
Matokeo ya ushindi au sare ya kuanzia mabao mawili yataihakikishia Yanga kutinga hatua ya makundi
Kocha Mwinyi Zahera amesema lengo kuu ni kupata ushindi na sio matokeo ya sare
Leo Yanga imefanya mazoezi yake ya kwanza nchini Zambia

No comments:
Post a Comment