Kiungo wa Kagera Sugar Gift Mauya amemuomba radhi kiungo mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib baada ya kumfanyia tukio lisilo la kiungwana kwenye mchezo baina ya timu hizo juzi
Mauya alimfanyia Ajib rafu za makusudi na pengine mwamuzi alistahili kumpa kadi nyekundu kwani alionekana alidhamiria kumfanyia Ajib madhambi hayo
"Nachukua nafasi hii kukuomba radhi rafiki,na mchezaji mwenzangu Ibrahim Ajibu kwa mchezo usio kuwa wa kiungwana hapo jana," ameandika Mauya kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
"Ni tukio ambalo hutokea ndani ya mchezo ikiwa umefungwa na damu ikiwa imechemka na pia niuombe radhi uongozi wangu wa Kagera Suger na Simba pamoja na mashabiki zangu kwa ujumla"
Juzi Ajib alikuwa na mchezo mzuri uliwapa wakati mgumu wachezaji wa Kagera Sugar ambao mara kwa mara walimfanyia madhambi
Kwenye mchezo huo Ajib alipata majeraha ya kuchanika ulimi ambapo kocha Patrick Aussems alilazimika kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Miraji Athumani
No comments:
Post a Comment