Mamia ya wahamiaji nchini Afrika wengiwao wakiwa ni kutoka Nigeria, Zimbabwe, Somalia na China wamekuwa wakionekana wakiyakimbia maduka yao tangu Jumapili iliyopita katika eneo lenye shughuli za kibiashara la Jeppestown Jijini Johannesburg kufuatia matukio yakuvunjwa kwa maduka yao na kuchomwa moto.
Ghasia hizo kwa sasa zimesambaa hadi kwenye maeneo mengine kama vile Denver, Malvern, Turffontein, Tembisa na maeneo mengine ya vitongoji vya jiji la Johansburg, Na wahanga wakubwa ni wahamiaji ambao wanashambuliwa na wazawa.
Wanawake na watoto ndio wamekuwa wahanga zaidi, Ambapo mpaka sasa watoto wanne wametekwa na watu wasiojulikana ambao wanataka walipwe Rand milioni 2 ambayo ni zaidi ya Tsh. Milioni 300 .
Katika kisa kingine, Mwanafunzi wa kike katika Chuo cha Kikuu cha Cape Town, Uyinene Mrwetyana alitekwa na Mfanyakazi mkubwa wa shirika la Posta nchini na kisha kubakwa na kuuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa vichakani.
Polisi mjini Johannesburg wamesema tayari wamewakamata watu 41 wanaotuhumiwa kuhusika na machafuko hayo ambayo hadi sasa watu wanne wameuawa, watatu wakiwa ni Wanaijeria.
Kwa mujibu wa Msemaji wa polisi nchini humo, Kapteni Mavela Masondo amesema kuwa maafisa wa polisi wamekuwa wakikabiliana na moto katika majengona Gereji zinazoungua moto huku wakiwatawanya wazawawanaochochea vurugu.
Bado hata hivyo, Polisi hawajapata taarifa za chanzo cha vurugu hizo na ni akina nani walioanzisha mashambulio hayo.
Waziri wa anayeshughulikia masuala ya Polisi, Bheki Cele amethibitisha kuwa waliovunjiwa maduka wengi ni Wanaijeria na amelaani ghasia hizo ambazo amesema hazina maana katika taifa hilo.
“Wakati bado tunafanya uchunguzi na huduma za dharura , Watu waliokuwepo karibu walianza kutumia fursa ya hali iliyopo na kupora maduka, Huu sio ubinadamu. Ninalaani vitendo hivi naomba tuungane kuwasaidia Waafrika wenzetu,“amesema Cele kwenye mahojiano yake na Kituo cha Taifa cha runinga cha SABC.
No comments:
Post a Comment